TANZANIA: “Nimeshindwa kuachia video, tatizo ni menejimenti” – Mo Music
1 April 2016

‘Basi nenda’ na Nitazoea’ ni nyimbo za Mo Music ambazo zimewahi kufanya vizuri katika media mbalimbali. Baada ya kupitia takribani miezi minne tangu atoe wimbo wa ‘Skendo’ amezidi kuwa kwenye hali mbaya baada ya kushindwa kutoa video yake. Akiongea na Bongo5 Mo Muic amesema, “Inaniuma sana nimeshindwa kuachia video ya skendo kwa wakati, tatizo ni menejimenti yangu”.
“Inaniuma sana na nimechoka kudanganya, kweli nimeshindwa kutoa video kwa wakati. Menejimenti yangu imenichelewesha kufanya hilo. Wiki ijayo nitaachia video mbili. Moja ikiwa ni ya video ya ‘Skendo’ na nyingine itakuwa ni ya nyimbo ynagu mpkya ambapo audio yake itafuata baadaye”.
Chanzo: Bongo5.com




Leave your comment