TANZANIA: Rachael aamua kumrudia Mungu.

 

Msanii kutoka katika nyumba ya kipaji ‘Tanzania House of Talent’ ‘THT’, Rachael amesema kuwa kwa sasa anamrudia Mungu. Akiongelea swala hilo katika mahojiano yake na Millard Ayo wa kipindi cha Amplifya kinachorushwa na Clouds Fm, Rachael alijibu na kusema kuwa, “ni maamuzi tu ambayo nimeyafanya, mwenyewe na kuona kuwa vitu ni vile vile , dunia ni ile ile na watu ni wale wale , kwahiyo nikaona si vizuri nikaja na upande mwengine”.

Aliulizwa kama kwa sasa anafanya Gospel, Rachael alijibu na kusema, “No, sifanyi gospel nafanya tu muziki wangu wa kawaida ila muda mwingi nautumia nikiwa kwenye kanisa.”

Akaulizwa kama ameamua kuokoka, Rachael alijibu na kusema, “ Sisi wasanii  huwa tunamsahau Mungu hata ile siku ya Ijumaa au Jumapili huwaga tunasahau, huwaga tuko bize sana na muziki, muziki huu wa kidunia. Japo hata siku moja ya Jumapili au Ijumaa si vibaya. Kuliko kukaa kufikiria jumapili hii naenda wapi, ijumaa nitakuwa klabu gani? Okay sawa klabu zipo lakini na Mungu naye mkumbuke”.

 

 

 

Leave your comment