Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
TANZANIA: “Sina bifu na Ommy Dimpoz” – Diamond
31 March 2016

Msanii Diamond Platnumz amesema hana bifu na msanii wa bongo fleva Ommy Dimpoz. Katika mahojiano yake na Millard Ayo, amesema kwamba yeye na Ommy hawana bifu la aina yeyote, sema tu kuna ukaribu kidogo umepungua.
“Mimi na Ommy Dimpoz hatujagombana sema kuna ukaribu kidogo tu umepungua”. Aliongeza Diamond na kusema, “Amefika kwenye sehemu nzuri sasa ni wajibu wangu kuwashika wengine mkono wafanye kitu kizuri na yeye aweze kuwashika watu wengine. Tukishikana sisi wenyewe kwa wenyewe tutakuwa wabinafsi, hatuwezi kukua na kuwasaidia watu wengine”
“Mimi kwa sasa niko na Harmonize na Raymond”, aliongeza Diamond. Diamond alisema kuwa ukaribu wake na Ommy umepungua kwasababu amekuwa akisafiri mara kwa mara na yeye Ommy anasafiri mara kwa mara pia, lakini hakuna bifu lolote kati yao.
Weekly Top 10 songs

Kamwambie3:47
chile-one-so-lucky4:02
Buwooma2:44
Joy Is Coming3:08
Nakupenda3:12
Udede Ft Msomali x Malume & Samas Alifata Hela Remix6:34
Msaliti 11:25
Paver2:55
Ssirivawo ft yven feiz2:10
Ziyakuba kabotu6:57
Top stories
- One and only
01 May
- SHUKRANI
02 May
- Okello oyumu
01 May


Leave your comment