TANZANIA: Msanii wa nyimbo za Injii ataka kufanya kazi na Diamond.
31 March 2016
Msanii wa nyimbo za Injili nchini Angela Magoti amesema kwamba anatamani sana siku moja aweze kufanya kazi na Nasib Abdul a.k.a Diamond Platnum, Rubi pamoja na Linah.
Msanii huyo ametoa ya moyoni alipokuwa akifanya mahojiano maalum katika kipindi cha eNews kinachorushwa na EATV na kubainisha wazi kwamba kuna umuhimu wa waimbaji hao kushiri kazi kumuimbia Mungu pia. ''Ninafanya strategies za kufanya kazi na Diamond Platnum kwani naamini kuna faida kubwa katika kumtumikia Mungu''Amesema Magoti.
Diamond Platnumz
Msanii huyo ameweka wazi pia kuwa na shauku ya kutengeneza wimbo na msanii wa bongo fleva Rubi pamoja na Lina kwani kuna watu wengi makanisani wanadhambi sana hivyo haoni sababu ya ni kwa nini asifanye kazi na wasanii hao kwa lengo la kumtukuza na kumwabudu Mungu.
Leave your comment