TANZANIA: Sababu za Juma Nature kusisitiza pambano kati yake na Diamond

 

 

Diamond Plutnumz ni msanii mwenye mafanikio makubwa sana hapa nchini Tanzania hii inatokana na juhudi zake katika kazi, umahiri wake wa kucheza jukwaani na kolabo nyingi alizofanya na wasanii mbalimbali barani Afrika akiwemo Davido, AKA, Mr Flavour, Waje, Akothee na wengine wengi. Umahiri huo na tuzo nyingi za ndani na nje ya nchi alizo nyakua zimepelekea Diamond Plutnumz kutajwa kuwa ndiye msanii bora nchini Tanzania, jambo ambalo limepelekea wasanii wengi kutaka kufanya nae kolabo, wakifikiri huenda wakatoboa kama yeye.

Kwa upande wake msanii Juma Nature ambaye aliwahi kutamba sana kipindi cha nyuma na vibao vyake mbalimbali kama Ugali, Sitaki Demu na vingine vingi ambavyo vilikonga nyoyo za mashabiki wake, hivi karibuni msanii huyo alikaliliwa na vyombo vya habari akiomba pambano kati yake na Diamond Plutnumz.  Baadhi ya sababu ambazo zimempelekea msanii huyo kuomba pambano na msanii huyo ni kile kinachodaiwa kuwa Diamond amekuwa akitukuzwa na kuonekana kuwa hana mpinzani katika tasnia ya muziki, jambo ambalo Juma nature ana amini sio kweli hivyo yeye ndiye mtu pekee anayeweza kupambana na msanii huyo.

“Watu wanamtukuza sawa lakini watuweke stage moja tuone nani atakamua, unajua tuseme ukweli Bongo Flava sasa mimi na Diamond ndio wapinzani pekee. “Watu waandae pambano, na mpunga pia uwepo nioneshe” alizungumza Juma Nature katika moja ya mahojiano yake. Usione vyaelea ujue vimeundwa, naimani umahiri wa Diamond ndio umempelekea Juma Nature kufunguka hayo yote huku akiwa na imani kuwa endapo pambono hilo litafanikiwa licha ya kuingiza mkwanja atakuwa amejipima na kutambua anakubalika kwa kiasi gani kwenye jamii, ukilinganisha enzi zake.

Chanzo: Mtembezi.com

 

 

Leave your comment