TANZANIA:”Sina mpango wa kutoa wimbo mwaka huu” – Roma
24 March 2016

Rappa Ibrahim Musa “Roma”, ameeleza kuwa hawezi kuisahau mwaka 2015, kwakuwa ni mwaka aliokuwa na mzuka wa ajabu wa kazi tofauti na mwaka huu.
Akizungumza na na Times Fm, Roma amedai kuwa kuna uwezekano mwaka huu asirekodi wimbo wowote ule. “Nilifanya kazi nyingi mwaka 2015, na nilikuwa na mzuka wa ajabu, yaani naweza mwaka huu 2016 nisirekodi kabisa”. Licha ya hayo Roma kwa sasa anatamba na wimbo wa Mtoto wa Kigogo aliomshirikisha staa wa shindano la kusaka vipaji Bongo Star Search BSS Walter Chilambo, huku akitamba na ngoma nyingine aliyo shirikishwa na rapa Baghdad inayoitwa Una Akili wewe?




Leave your comment