TANZANIA: “Ninampango wa kuitoa familia yangu kijijini” - Harmonize

 

Harmonize anang’ara kwa sasa lakini safari yake lakini safari yake hadi kufikia hapo alipo leo imekua ni ngumu na yenye misukosuko mingi. Ni msanii anayetoka katika maisha magumu katika kijiji chao kilichopo Tandahimba, mkoani Mtwara kwenye familia kubwa yenye wake wengi ambayo baba yake ni sheikh. Kwa mama yake walizaliwa watoto watatu huku yeye akiwa ni mtoto wa pili kuzaliwa. Baba yake anawake wengine watatu na watoto wanane lakini aliachana na mama yake akiwa bado ni mtoto kwahiyo amekulia kwenye familia yenye mama tu.

“Mimi nimezaliwa Bush kweli hata umeme hatuujui, mimi nimekuja town mwaka 2009 tu” anasema.  Hiyo ni baada ya kushindwa kuendelea na sekondari, baada ya kuishia kidato cha tatu  na kutokana na baba yake kupendelea wanae wasome elimu ya akhera ( elimu ya dini ya kiislam). Dar alifika kwa dada yake ambaye baada yake ambako baada ya muda alijikuta akipishana na shemeji yake na kuamua kuanza kuishi mwenyewe kwa kufanya kila kibarua kinachojitokeza mbele yake. Kuna wakati alikuwa akilala kwenye stendi ya mabasi ya mkoa Temeke.

Wakati huu ambao maisha yanabadilika baada ya kusaini WCB, Harmonize hajaisahau familia yake na ana mipango mikubwa. “Ninafanya mpango familia yangu nije niishi nayo hapa, kwasababu kijijini kwetu kuna mazingira magumu sana sidhani kama mtoto mwenye akili timamu unaweza ukafurahia aishi maisha ya tabu wakati wewe unaishi maisha mazuri”, alisema Harmonize. “Nilikuwa nafanya mpango panapo majaaliwa nilikuwa naongea na management yangu ili niwe comfortable zaidi hata familia yangu isogee hapa”.

 

Chanzo:Bongo5.com

Leave your comment