TANZANIA: “Wasanii wengi wamesahau kuandika nyimbo za kuigusa jamii”- Bonta
23 March 2016

Bonta ni moja kati ya wasanii wa hip hop hapa nchini Tanzania, mwenye uwezo wa kuandika mistari inayoweza kuchukuwa muda mrefu kufikirika na kuchukua muda mrefu kukielewa ktu anachokimaanisha.
‘Kura yangu’, ‘Nyerere’ ni moja kati ya nyimbo ambazo ameshawahi kuziachia kwenye media na kufanikiwa kutoa somo kubwa kwa jamii. Hivi karibuni aliachia wimbo uitwao ‘Usirudi Jela’.
Akiongea na Bongo5 wiki hii Bonta alisema , “Watu wanatakiwa kurudi misikitini na makanisani lakini wasiombe kurudi jela”.
“Wasanii wengi wamesahau kuandika nyimbo za kuigusa jamii nyimbo kam ‘Mchizi wangu’ zilikuwa za mwisho. Pia kwenda jela sio kwamba ndio umeharibu kila kitu, wapo wengi wameenda jela na wameweza kufanya vitu vikubwa. Mfano Lulu aliennda jela kwa kesi ya Kanumba, lakini ameweza kutka na kupambana na hivi karibuni alifanikiwa kupata tuzo na kuitangaza nchi” ameongeza.
“Kwenye wimbo wangu usirudi jela alitakiwa kufanya Jux na sio Belle9, kwa kuwa Jux alikuwa bize sana Gnako akanishauri hata Belle9 anafaa kwa kuwa wote ni familia ya Weusi”.
Bonta kwa sasa anafanya mpango wa kuongea na baadhi ya wadau ili aandae Documentary ya wimbo wake huo.
Chanzo: Bongo5




Leave your comment