TANZANIA: Diamond azidi kushow love kwa familia yake
23 March 2016

Familia ni kitu cha kwanza kwa Diamond. Familia inapaswa kuwa kitu cha kwanza kwa kila mtu. Watu wake wa muhimu kwenye maisha yanke ni mwanae Tiffa, Mpenzi wake Zari Hasaan na mama yake Sandra. Wakati Diamond akiendelea na safari zake za Ulaya aliyoipa jina #FromTandaleTo WorldTour, msanii huyo ameona ni vyema aichukue familia yake na kuzunguka nayo. Anazunguka na timu kubwa. Ukiitoa familia yake Ofcourse bila kumsahau Binamu yake Rommy Jones, Diamond ameenda Ulaya akiwa na dancer wake wane, mpiga picha, meneja (wanapokezana Sallam Sk pamoja na BabuTale) na watu wengine wawili akiwemo mke wa Tale.
Ni msafara mkubwa ambao sehemu yake bila shaka haupo kwenye bili anazotakiwa kugharamikia Promota wa show husika. Kimsingi inaonekana wazi kuwa Diamond anatumia muda huo pia kufanya vacation pamoja na familia yake. Hiyo anamaanisha kuwa anatumia gharama kubwa katika ziara hiyo. Hata hivyo kwa fedha anazoingiza kutoka kwenye Vyanzo lukuki, gharama hizi ni kama tone kwenye ndoo ya maji. Mtandao wa Global Publishers umedai kuwa ziara hiyo imemgharimu takribani shiingi millioni 100. Makadirio hayo yanaweza yakawa ni makubwa sana lakini ukweli ni kwamba anatumia gharama kubwa na ni ziara ya kifahari.

“Diamond ameandaa mkwanja usiopungua shilling millioni 100, kwa ajili ya msafara wake. Fedha hizo zitatumika kuanzia usafiri kwenda na kurudi, chakula, shopping na malazi kwa kipindi cha muda wa wiki 3 atakachokuwa ulaya”, mtandao huo umekinukuu kituo kimoja. GPL imedai imezungumza na msanii huyo na kujua kama kweli gharama zimefika: “Siwezi kusema moja kwa moja kama inafika au la lakini inaweza kufika na hata zaidi. Wewe chukulia mimi tu na familia yangu (yeye, Tiffah, Zari na ndugu zake) nimetenga kama dola 30,000 (zaidi ya Sh. milioni 65) kwa ajili ya usafiri, malazi na shopping za hapa na pale sasa vipi kuhusu timu nzima ya madansa, meneja na wengine?” wamemnukuu Diamond.
Kwa vyovyote vile huu ni wakti wake wa kula matunda ya jasho lake, na kama unaweza kuweka tabasanu kwenye sura za uwapendao, hakuna jambo kubwa linguine zaidi ya hilo.
Chanzo: Bongo5.com




Leave your comment