TANZANIA: “Picha ilisababisha nikaachana na mzazi mwenzangu”- Dayna
23 March 2016

Msanii wa muziki Dayna Nyange amedai kilichosababisha akaachana na mzazi mwenzake ni wivu wa kimapenzi kutokana na picha aliyopiga na Wahu, Prezzo pamoja na AY. Muimbaji huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwae Rahma, ameliambia gazeti la Mtanzania kuwa picha hiyo aliyopiga na wasanii hao kabla hajawa maarufu na kabla hajajihusisha katika muziki hivyo hiyo ilikuwa sehemu ya kutafuta marafiki wa kumsaidia kimuziki.
“Kutokana na picha hiyo mchumba wangu huyo alihisi kuwa mmoja ya wasanii hao labda natoka nao kimapenzi hivyo akawa hataki nipige picha na wasanii na nisijihusishe tena na maswala ya muziki”, alisema Dayna.
“Muziki ni kitu ninachokipenda sana katika maisha yangu hapo nikaona wivu umezidi kwa mwenzangu ambaye tumebarikiwa kupata mtot mmoja mwenye umri wa miaka 10, tukaamua kuachana nami nakendelea zangu na muziki hadi leo bila mchumba, mpenzi wala nini na maisha yanaenda”, alijieleza mrembo huyo.
Dayna alianza kujulikana katika muziki mwaka 2008 baada ya kuachia nyimbo ya ‘Mafungu ya Nyanya’ ambao alimshirikisha Marlow, kisha akatoa ‘Nivute Kwako’ na sasa anatamba na ‘Ungejua’.
Chanzo: Bongo5.com




Leave your comment