TANZANIA: Jay Dee ajibu tetesi za kurudiana na Gardner.
23 March 2016

Msanii mkongwe katika muziki wa Bongo Fleva, Lady Jay Dee amefunguka kuhusiana na tetesi kwamba amerudiana na aliyekuwa mume wake Gardner G Habash. Lady Jay Dee aliulizwa swali hilo na Sam Misago katika kipindi cha Enews kinachorushwa na Eatv na kusema, “Watu wengi walinipenda kama nilivyo na hawakunipenda nikiwa na mtu yoyote, sipendi kuelezea mambo yangu binafsi, naomba watanzania wanipende kama mimi kama Jay Dee na si vinginevyo”.

Lady Jay Dee akiwa na aliyekuwa mumewe Gardner G Habash siku ya ndoa yao
Msanii huyo ameibuka tena na wimbo wake Mpya uitwao ‘Ndindindi’ ambapo amesema video yake ataitoa itakapokuwa tayari.
Chanzo: Bongo5.com




Leave your comment