TANZANIA: “Namuadmire WizKid” – Linah

 

Baada ya hivi karibuni kumsikia msanii wa Kenya Kelvin Bahati kusema  kwamba huwa anatamani angekuwa na mahusiano na msanii wa bongomovie Elizabeth Michael ‘Lulu’, Msanii wa muziki wa bongo fleva nchini Tanzania, Linah Sanga amesikika nae hivi karibuni akisema anatamani kuwa na msanii wa Nigeria, Ayojedi IbrahimBalogun almaarufu kama ‘WizKid’.

 

 

 

 

 

Katika mahojiano yake Linah kwenye kipindi cha Enews kinachorushwa na kituo cha Eatv na kusema, “ unajua nilikuwa namuadmire WizKid tokea muda mrefu, na ndio mwanaume hata ukiniuliza ni msanii gani wakiume katika bara la Afrika ambaye ungependa kuwa naye au ambae nampenda nitakwambia ni WizKid, siwezi kukataa ila ndiyo hivyo tena maana mwenyewe natamani ingekuwa kweli”, alisema Linah Sanga.

 

 

 

WizKid

 

Katika hatua nyingine msanii huyo kwa sasa anasema ameamua kufanya tu kazi na kuachana na masuala ya mapenzi na kusema kuwa akichanganya kazi na mapenzi mwisho wa siku hata kazi yenyewe anaweza kuharibu. Linah amedai mpaka sasa ana mipango ya kufanya kazi na Wizkid ingawa anadai kwa sasa alimwambia yupo 'busy' kidogo mpaka siku za usoni ndipo wanaweza kukamilisha kazi hiyo.

 

 

Leave your comment