TANZANIA: Babutale ampeleka Chidi Sober House

 

Msanii wa miondoko ya hip hop Chidi hivi karibuni aliomba msaada kutokana na hali yake kudhoofika. Msanii huyo aliyazungumza hayo wiki iliyopita kupitia kipindi cha The Weekend Chat Show kinachorushwa hewani na Clouds Tv, ambapo aliomba msaada wa kusaidiwa kutokana hali yake kudhoofu kwasababu ya matumizi ya madawa ya kulevya.

Meneja wa Diamond, BabuTale ni moja kati ya wadau wa muziki hapa nchini Tanzania, hivi karibuni alionekana kujitolea kumsaidia  msanii huyo aliyepatwa na matatizo hayo. Babutale akishirikiana na Kalapina wamemchukua Chidi Benz na kumpeleka Life and Hope Rehabilitation Organization iliyopo Bagamoyo kwa ajili kumsaidiwa kuacha matumizi ya madawa ya kulevya.

 

 

 

 

Babutale katika mtandao wa kijamii wa Instagram alipost video na kusema,"Mwana amekubari kukaa Soba ila anasisitiza wana mje kumtembelea kumpa hope na kuleta mapokopoko manjari. Mungu bariki hii safari ya matumaini"

Leave your comment