TANZANIA: Babutale ajitoa kumsaidia Chidi Benz
22 March 2016

Picha zilizosambaa za msanii huyo wa kundi la La Familia Chid Benz zilwshtua watu wengi. Chidi Benz alikiri kuwa anahitaji msaada kwani hayuko vizuri. Na sasa huenda msaada anotaka umepatikana. Babutale amepost video Instagram akiwa na rapa huyo akisema: “Mungu tusimamie, tusaidie mjaalie Tale nijaalie na mimi, tunaomba mengi, tutakuwa na vingi, tutaenda sehemu nyingi tutafanikiwa”, na Tale alimalizia na kusema, “ inawezekana, Chidi kaamua”. Haijulikani hasa ni nini kimepangwa kufanyika lakini la msingi ni kuwa umoja wa wasanii umeonekana kutokumwacha Chidi apotee.
Hata hivyo katika hatuailiyowashangaza wengi, rappa Young Dee ametupia lawama kwa kuweka video hiyo.

“Nimeiona hii post nikajiuliza, Kwa hali kama hii sio mwanzo mzuri kama ni mwanzo wa kumsaidia Chidi.. Haonekani vizuri.. Challenge kwako blaza hii ni aibu sidhani kama kuna die hard fan wa ukweli wa Chidi Kama ataipenda hii au hata kama ni kweli unampano wa kumsaidia kama manager bora Afrika…! Nimeiona hii nimestuka Tale! @babutale umeniangusha kwa hili.. Starting to healbut kill the best rapper mbele ya macho ya waTz”
Umemuelewa Young Dee?
Chanzo: Bongo5.com




Leave your comment