TANZANIA: “Sipendi kuhusishwa kwenye Skendo za Wanawake” – Harmonize

 

Harmonize kutoka WCB anasema kwa jinsi alivyolelewa na wazazi wake hapendi kabisa kuwa na skendo za wanawake.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo wa ‘Bado’ aliyomshirikisha Diamond Platnumz, amekiambia kipindi cha ‘Playlist’ cha Times Fm kuwa akianza kuwa na skendo za wanawake wazazi wake wataanza kumfikiria vibaya.

“Unajua mimi siku zote nakataaga kuzungumzia maswala ya mahusiano, kwasababu mimi nimetoka katika familia ya kimaskini sana halafu inavyokuja umaarufu familia yangu inatarajia kwamba itapata rizizki kupitia mimi, so leo labda kukitapakaa taarifa kuwa Harmonize yupo na huyu, sijue yupo na huyu sidhani kama familia yangu itanielewa, wao watajua pesa ninazopata kwenye muziki  nazimaliza kwa wanawake”, alisema Harmonize.

“Halafu mama yangu alikuwa akinisapoti sana kwenye muziki wakati naanza. So akiona nipo na wanawake anaweza akakunja moyo basi huyu asifanikiwe”, aliongeza Harmonize.

Pia Harmonize alisema video yake na Huddah ambayo ilisambaa katika mitandao ya kijamii ilikuwa ni project na aliamua kuifuta isije ikamletea matatizo.

 

Chanzo: Bongo5.com

Leave your comment