TANZANIA: Harmonize awa Balozi wa WWF
22 March 2016

Muimbaji wa ‘Bado’ Harmonize akteuliwa kuwa Balozi wa Taasisi ya utunzaji mazingira World Wide Fund For Nature ‘WWF’ kwa Tanzania.

Harmonize akisaini mkataba
Muimbaji huyo alisaini mkataba wa ubalozi huo wiki iliyopita kwenye Taasisi hiyo zilizopo Mikocheni, Dar Es Salaam. Kama sehemu ya ubalozi huo, Harmonize alihudhuria makabidhiano ya mradi wa maji unaotokana na nishati ya jua huko Kigamboni Jumamosu iliyopita. Kabla ya Harmonize Ubalozi huo ulienda Kwa Rich Mavoko.

Harmonize akiwa na Timu ya WWF
Chanzo: Bongo5.com




Leave your comment