TANZANIA: Diamond ampost Bob Juniour

 

Itakumbukwa #Nenda kamwambie ambayo ilipikwa na Prodyuza Bob Junior chini ya ‘SHAROBARO RECORDS’ ndio ngoma iliyomtoa Diamond Platnumz  katika uso wa sana ya muziki wa kizazi kipya Tanzania hadi sasa ulimwenguni, Lakini baada ya kuanza kufanya vizuri wawili hao walitofautiana kama ilivyo kawaida kwa binadamu.

 

Kimsingi tofauti zao zilianza baada ya kutoa vibao kadhaa ikiwemo ile ya #Mbagala baada ya hapo Dimond akaanzisha jina la wasafi na Bob junior akabaki kuitwa Sharobaro huku katika nyimbo zake bob junior alikuwa anasema kuwa yeye ni raisi wa wote kuanzia wasafi hadi sharobaro wote mjini

 

Katika hali ambayo haikuitarajiwa hivi karibuni katika ukurasa wa Instagram ‘ICON’ wa Tanzania kupitia muziki wa bongo fleva DIAMOND PLATNUMZ ameposti picha kumtakia kila la kheri katika siku yake ya kuzaliwa mtayarishaji wa ngoma yake ‘Nenda kwamwambie’ BOB JUNIOR ambapo leo prodyuza huyo na msanii wa bongo fleva ana sherehekea siku yake ya kuzaliwadiamondplatnumz

 

 

 

Diamond ameandika maneno haya “A major Happy Birthday kwa mmoja wa watu wenye mchango mkubwa kwenye career yangu…@bobjuniortz let`s drop our wishes my people akamaliza hivyo DiamondMashabiki wa Diamond platnumz wameonekana kuipokea kwa hisia nzuri ujumbe huo ambapo Diamondi ame ‘mtag’ Bob junior katika post hiyo

Diamond alishawahi kusikika katika mahojiano yake kuwa kuna mzigo upo ambao ataufanya na producer huyo hivyo kinacho subiriwa na muda kuweza kufanya vitu hivyo.

 

 

Chanzo: mtembezi.com

Leave your comment