TANZANIA: Chidi Benz asaidiwe, kuteleza si kuanguka.
21 March 2016

Katika mitandao ya kijamii jumamosi iliyopita kulisambaa picha za rapa Chidi Benz ambazo zinamuonyesha jinsi alivyokonda na kupoteza ule mwili wake wa kuvutia aliokuwa nao zamani.
Mkali huyo wa nyimbo ya ‘Dar es Salaam Stand Up’ anakubalika na vijana wengi kutokana na uwezo wake wa kuandika na kuchana. Lakini miaka ya hivi karibuni alianza kubadilika baada ya kujiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.
Oktoba 24, 2014 Chidi alikamatwa na madawa ya kulevya katika uwanja wa J. K Nyerere wakati akielekea jijini Mbeya kwa ajili ya show. Lakini kesi hiyo ilimalizika miaka michache baadae baada ya kuamriwa na mahakama kulipa faini.
Tukio hilo liliwafanya wasanii mbalimbali kuzungumzia hali hiyo huku wakimshauri kuachana na madawa ya kulevya. Ray C ambao ni moja kati ya waathirika wa janga hilo ambae kwa sasa yuko kwenye tiba ya Methadone aliamua kumshauri Chidi Benz.
“Pole kaka yangu Chidi. Naumia kuona tatizo ulionalo bado hujaamua kulitafutia jibu la kutatua tatizo lako. Mimi ni dada yako natumeshafanya kazi pamoja, tatizo ulilonalo nilishakuwa nalo na niliweza kulitatua baada ya kujitambua an kutafuta suluhu. Nimejaribu kila njia kukushauri badala yake ulinijia na rungu la kimasai kunitandika nalo nyumbani”, aliandika Ray C kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Hata hivyo hidi Benz aliendelea na harakati zake huku akijinadi kwenye vyomb vya habari kuwa ameshaachana na madawa ya kulevya. Lakini watu wake wa karibu pamoja na marafiki zake walidai kwamba bado hajaacha. Lakini jumamosi hii katika kipindi cha Da Weekend Chat Show kinachorusha katika kituo cha utangazaji cha Clouds Tv, Chidi ameonekana amechoka Zaidi na ameomba wadau wamsaidie.

“Matatizo yangu na Stress zangu zinasababisha mwili wangu kupungua siko okay, siko poa, siko sawa yaani”, alisema Chidi.
Mmoja kati ya wasanii wakongwe wa hip hop, Afande Selle alionyesha kusikitika na jinsi madawa ya kulevya yanavyomaliza nguvu kazi za taifa. “Yanapita kwa njia gani haya madawa ya kulevya hapa nchini? Anayasambaza nani mtaani? Madawa ya kulevya hayaleti maendeleooo, madawa ya kulevya yanauwa masala leooo”, alisema Afande Selle.
Pia wadau mbalimbali wamewataka watu pamoja na wasanii wenzake kumsaidia, huku Arnold Kayanda mtangazaji wa BBC Swahili amesema amelipokea kwa masikitiko makubwa.
“Kama picha hii ni rafiki yangu Chidi Benz kama nilivyotaarifiwa, kwa hisani yetu wote naomba kila mtu kwa uwezo wake amsaidie. Mimi niko mbali nikirudi nitakutana nae”.
Licha ya wadau mbalimbali wakitaka wamsaidia, lakini bado tunaona hakuna msaada wa haraka ambao mpaka sasa umecukuliwa ili kumuokoa Chidi Benz. Serikali ya Magufuli ni sikivu sana Bilas haka kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inayoongozwa na Waziri kijan a mpenda Sanaa, Nape Nnauye ataliangalia hilo.
Chanzo: Bongo5.com




Leave your comment