TANZANIA: Ben Pol aleleza sababu ya nyimbo yake kuchezwa katika runinga za nje.

 

 

Msanii wa muziki wa R&B Ben Pol baada ya video yake ya wimbo wa ‘Ningefanyaje’ kuchezwa mara kadhaa katika runinga za kimataifa, ameeleza vitu muhimu ambavyo vimeweza kusababisha video hiyo kuchezwa katika runinga za kimataifa.

Akizungumza na Bongo5 jumatatu hii, Ben Pol, amesema video yake ilikuwa inasifa tatu muhimu. “Kwanza nimegundua kuna vitu vitatu muhimu sana, na kati ya hivyo sikuja ni kipi kimesababisha kazi yangu kupata airtime, lakini kwasababu imechezwa naweza sema vitu vitatu muhimu, alisema Ben.

“Moja ni ubora wa kazi, ubora wa video yangu ulikuwa mzuri sana na ndio aina ya video wanazozipiga wao kila siku. Kigezo cha pili ni kutoacha kuwasumbua na kuwakumbusha, mbona kimya, sababu mimi video yangu niliituma mwaka jana mwishoni, lakini baada ya kuwakumbusha mara kwa mara wameanza kuicheza mwezi wa pili mwaka huu, kwahiyo kilichonisaidia mimi. Kitu cha mwisho ni connection ni ya director, director niliyefanya nae (Justin Campos) tayari anatambulika na kuna kazi nyingi amefanya na zinafanya vizuri. Kwwahiyo kwa upande wangu hivi ndivyo vitu muhimu kama unataka video yako ichezwe katika runinga za kimataifa” aliongeza Ben.

 

Leave your comment