TANZANIA: “Sina beef na Vanessa” – Shaa
18 March 2016

Hakuna kitu kinachomuumiza Shaa kama tetesi za yeye kuwa na beef na Vanessa. Akiongea na Bongo5 Shaa amesema anaamini kuwa vyombo vya habari vinajaribu kutengeneza beef ambayo haipo. Shaa anasema mwanzoni alisikia tetesi hizo kwa Soudy Brown wa Clouds Fm aliyemtaka athibitishe kama kitendo cha Vanessa kutumia dancer wake kilimkera.
Alisema alikuwa hana tatizo na hilo kwakuwa anafahamu kuwa wasichana hao wengine wanafamilia na wapo mjini kutafuta maisha hivyo ni ikitu alichokiunga mkono na hakuwa na sababu ya kuwazuia. Anadai pamoja na kujaribu kuzima tetesi hiyo baadae vyombo vya habari viliendelea kuikuza kitu amabacho anadai hakukipenda.
“Mara mia watu wangebishana kwanini hakuna featuring ya Shaa na Vanessa kuliko kutugombanisha”, amesema Shaa.
“Kwangu mimi Vanessa kufananishwa na mimi simind ilimradi unanifanisha nae kwa namna nzuri, usinifananishe kiushindani sababu sisi ni watu wawili tofauti, ni wasanii wawili tofauti. Nimekuwa nikijaribu kuizima na imekuwa ikinikera. Inanikeera kwasababu wanatushindanisha badala ya kutuhamasisha, ukizingatia wasanii wanawake tuko wachache sana”, ameongeza Shaa.
Chanzo: Bongo5




Leave your comment