TANZANIA: Matumizi mengine ya Instagram- Nuhu Mziwanda.

 

 

Mitandao ya kijamii ina maana kubwa kwa wasanii kutokana na kutumiwa na watu mbalimbali hivyo wasanii hutumia mitandao hiyo kutangaza kazi na maisha yao ya kila siku, vilevie kuna faida na hasara ya kutumia mitandao ya kijamii inategemea na matumizi ya muhusika, Nuhu Mziwanda anafunguka zaidi kuhusiana na suala la mitandao ya kijamii hususani Instagram.

Akizungumza na Planet Bongo ya East Afrika Radio Nuhu Mziwanda ameeleza kuwa anatumia mitandao ya kijamii kwa kwa madhumuni mbalimbali licha ya kutangaza kazi zake na kuonesha maisha yake binafsi staa huyo ameeleza kuwa kwa upande wake huwa anajitahidi kupost vitu vya kuelimisha jamii kwa mashabiki wake ili waweze kujifunza kwa namna moja ama nyingine.

 Hitmaker huyo wa Hadithi ameongeza kuwa angependa kuona kwa wasanii wenzake na jamii kwa ujumla wakipost vitu vyenye tija ambavyo vitaleta mabadiliko chanya kwenye jamii inayo wazunguka.

 

Chanzo: Mtembezi.com

Leave your comment