TANZANIA: "Nikimpata Lulu, nitatulia kabisaaa" - Bahati

 

 

Msanii wa nchini Kenya ameamua kutoa ya moyoni juu ya mrembo anaeiwakilisha vizuri tasnia ya maigizo ya nchini Tanzania Elizabeth Michael. ametokea kupendwa na muimbaji wa nyimbo za dini wa nchini Kenya aitwae Kelvin Bahati.

Elizabeth Michael 'Lulu'

 

Katika mahojiano ya  Bahati na Mseto’s Melody Sinzore ndani ya kipengele cha  #TatuChachu Mambo Mseto ya nchini Kenya, Msanii huyo wa nyimbo za dini alikiri na kusema kuwa amejikuta akiwa na hisia za kimapenzi kwa Lulu. Bahati alisema, “Nikiweza Mpata LULU ELIZABETH MICHAEL Nitatulia Kabisaaaaa , Mtaacha Kusikia Nikiitwa Single Boy, MILLARD AYO akileta #StoryZaBongo Mwambieni Nimemtuma apeleke hizi habari kwa ELIZABETH MICHAEL”. Bahati kwa sasa yuko nchini Marekani.

 

Lulu hivi karibuni alitoka kushinda Tuzo za AMVCA zilizofanyika nchini Nigeria.

 

Chanzo: Msetoea.com

 

Leave your comment