TANZANIA: Hiki ndicho kilichomvutia Kanye West kwa Diamond.
17 March 2016

Hivi karibuni picha zilisambaa mtandaoni zikionyesha msanii Diamond Platnumz akiwa na rappa wa kimarekani anayetamba sana duniani Kanye Omari West. Kanye west ni mwanamuziki wa miondoko ya hip hop, pia ni mjasiliamali, mwanamitindo na ni muandishi wa nyimbo.
Diamond Platnumz alipost picha hiyo akiwa na Kanye West siku chache zilizopita. Katika mazungumzo yake na kipindi cha Planet Bongo kinachotangazwa na Dullah katika kituo cha habari cha East Afrika Radio, Diamond Platnumz alisema, “Kanye West alivutiwa na viatu nilivyokuwa nimevaa”. Diamond aliendelea na kusema, “ Nilipokuwa airport pale Los Angels tunasubiri kuchukua mabegi yetu, nikasikia mtu akisema ninaweza kupiga picha viatu vyako? Kwakuwa alikuwa ameinama sikuweza kumtambua, lakini alipoinuka nilishangaa kumuona ni brother Kannye West. Nilimuomba tupige picha kwanza halafu vingine vitaendelea”.
“Tumuombe Mungu mambo yaendelee vizuri kama tulivyopanga, kuna kitu kizuri kinaweza kikatokea kati yetu”, aliongeza Diamond.




Leave your comment