TANZANIA: Ruby asingekuwa na management tungemchukua – Babu Tale

 

Meneja wa msanii mahiri wa msanii Diamond Plutnumz maarufu kama Babu Tale amefunguka kuhusu projects mbalimbali za lebo ya WCB na kueleza wamejipanga kuibua vipaji vipya bila kubagua jinsia na kusajili wasanii wakubwa kwenye lebo hiyo ili kupanua wigo wa kibiashara na tasnia ya muziki.

Ruby

 

Akizungumza suala la kuibua vipaji bila kubagua jinsia meneja huyo ameeleza kuwa wanahitaji kuibua vipaji vya wanawake kwasababu kuna wanawake wachache wanaotamba kwenye ramani ya muziki, hivyo wanahitaji msanii wa kike mwenye uwezo kama wa Rubby au zaidi ya hapo, huku akieleza kuwa Rubby angekuwa hana menejimenti wangemchukua kwenye lebo ya WCB.

 

Rich Mavoko

Kuhusu suala la uvumi wa msanii Rich Mavoko kuhamia kwenye lebo ya WCB Babu Tale ameeleza kuwa utakapo fika wakati muafaka uongozi wa WCB utaeleza kuhusu ujio wa msanii huyo mwenye sauti ya kuvutia.

 

 

Leave your comment