TANZANIA: Raymond ni msanii mpya kutoka kwenye lebo ya WCB

 

 

Siku chache zilizopita msanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ alipost katika mitandao ya kijamii kupitia Instagram pamoja na Twitter na kuandika kuwa siku chache zijazo watamtambulisha msanii mpya. Na hivi leo katika kipindi cha Leo Tena kinachorushwa na kituo cha habari cha Clouds Fm kimemtambulisha rasmi msanii Raymond na pia ameachia nyimbo yake iitwayo “Kwetu”.

 

 

Wasafi Classic Baby

 

 

Kipaji cha Raymond kilianza kuonekana mwaka 2011 baada ya kushiriki kwenye mashindano ya FreeStyle mkoa wa Mbeya na kuwa mshindi wa kwanza,alipokuja Dar akaibuka pia mshindi ndipo TipTop Connection ilipomchukua na kuwa chini yake,Raymond ameshaonekana kwenye majukwaa mengi hasa kwenye show za Madee,Kutokana na ukaribu wa Lebo ya TipTop Connection na WCB,Menejimenti zimekaa chini na kukubaliana kumtoa kupitia lebo ya WCB.

Unaweza kuisikiliza ngoma hii hapa:

Chanza: Millardayo.com

 

Leave your comment