TANZANIA: Kayumba aelezea jinsi alivyotumia mil 50
16 March 2016

Mshindi wa shindano la kutafuta vipaji vya kuimba, Bongo Star Search ‘BSS’ Kayumba Juma ameelezea kile ambacho amekifanya kwa kutumia zawadi aliyoshinda kwenye shindano hilo mwaka jana.
Kayumba alishinda kitita cha shilingi millioni 50. “Sasa hivi nina maisha yangu, nina miliki gari yangu mwenyewe, usafiri, halafu vile vile ninamalizia nyumba yangu najenga kwahiyo nashukuru kwa hilo, ila nawashukuru sana wananchi kwa kuniweka hapa”, ameiambia Bongo5.
Amewaomba mashabiki wake waendelee kuunga mkono kazi zake, na ameahidi hatowaangusha. Hivi karibuni aliachia video yake mpya iitwayo “Katoto” iliyofanyika nchini Afrika Kusini.
Kama hukupata fursa ya kuitazama unaweza kuiangalia hapa:
Chanzo: Bongo5.com




Leave your comment