TANZANIA: Baraka aelezea sababu ya kutokufanyika kwa kollabo mbili ikiwemo ya staa wa Nigeria.
15 March 2016

Najua nina watu wangu ambao mnafuatilia muziki wa Baraka Da Prince kama unakumbuka mwaka jana aliwahi kufunguka kwenye vyombo mbalimbali kuhusu kufanya collabo na staa Eddy Kenzo wa Uganda na Patoranking wa Nigeria.
Sasa leo March 15 alipokutana na ripota wa millardayo.com ametoa sababu ya kilichopeleka kwa kutofanyika kwa collabo hizo mbili na kusema…’Ni kweli Collabo zilitakiwa zifanyike lakini sema baada ya kuwa na uongozi mpya sikuweza kufanya collabo na Eddy Kenzo na Patoranking hiyo ndio ilikuwa sababu kubwa na kila kitu kilikuwa kimefanyika kilichobaki ni mimi tu kufanya nao sema kilichosababisha ni kuwa na uongozi mpya kwani uongozi wa zamani ndio walikuwa wamepanga collabo hizo‘Baraka Da Prince
Chanzo: Millardayo.com




Leave your comment