TANZANIA: Vanessa haamini kama nayeye angeweza kutoa ajira kwa wengine.

 

Hujafanikiwa bado kama huna uwezo wa kumuweka mtu mwingine mjini. Hujafanikiwa bado kama hujaanza kutengeneza ajira kwa vijana wenzako. Kwa wengi bado wanategemea kuajiriwa lakini kwa wale wanaojituma, lleo wametoka kwenye kuajiriwa na sasa ndio wanaoajiri. Vanessa Mdee ndiyo mmoja wao.

Miaka mitatu mine iliyopita, Vee Money alikuwa mwajiriwa kama vijana wengine. Alitegemea mshahara kutoka kwenye kazi yake ya utangazaji wa Tv kwenye kituo cha MTV Base na Choice Fm. Kwa wengi waliamini kuwa kipato alichokipata kwenye kazi hizi mbili nzuri kilimtosha kutimiza kila kitu anachokitaka.

Laahasha, Vee Mony alitaka makubwa Zaidi na ndio maana aliifufua career yake ya muziki ambayo mwanzo wakati anaanza wengi walikuwa na mashaka nae. Ni kwasabau watangazaji wachache waliingia kweny muziki na walifanikiwa.  Vee alikuwa determined, ndio maana baada ya kuona kuwa hawezi kutumikia mabwana wawili aliamua kuacha utangazaji na kuanza kufanya muziki 100%.

Huo ulikuwa ni uamuzi bora kuwahi kufanya kwenye maisha yake. Leo hii Vee ni msanii namba 1 kwenye Afrika Mashariki. Anashow kibao ndani na n je ya nchi. Na sasa amefikia kwenye mafanikio niliyoandika kwenye aya ya kwanza, kuweza kutoa ajira kwa wengine.

“Mungu ni mwema sana eti leo na mimi natoa ajira kwa watu. Dah #NeverEver Give up #ComeDanceWithVee  #VeeMoneyDanceAudition

 

Vanessa akiwa na majaji katika usaili

 

Baadhi ya vijana waliojitokeza katika usaili huo

 

Muimbaji huyo alifanya usaili wa kupata dancers watakao kuwa chini ya lebo yake Mdee Music. Inamaanisha dancers hawa watapata ajira kupitia vipaji vyao. Hongera Vanessa kutumia kipaji chako kutoa ajira kwa vijana wenzako.

 

Chanzo: Bongo5.com

Leave your comment