TANZANIA: Mambo 11 yawezekana huenda ulikua hujui kuhusu Shaa
15 March 2016

Kuna mambo 11 yawezekana ulikua hujui kuhusu Shaa, kupitia kipindi cha Chill n Sky unaweza kupata mambo 11 yanayomuhusu Shaa.
- Alizaliwa mwaka 1985
- Mtoto wa mwisho kwenye familia ya watoto wanne
- Baba yake ni mzaliwa wa Kyela, mama yake ni mzaliwa wa Nachingwea.
- Anatoka kwenye familia ya kimuziki, kaka yake ni mwanamuziki wa reggae, dada yake Nelly Kaisi ni mpiga gitaa la base.
- Baba yake, Dr Kaisi (amestaafu mwaka 2015) ni binwa wa magonjwa ya wanawake Tanzania. Alikuwa akiwatibu wake wa maraisi Tanzania.
- Mama yake alikua Kabidhi Wasii Mkuu wa Serikali wa kwanza mwanamke.
- Akiwa amemaliza kidato cha nne hakuwa amepanga kushiriki katika Coca Cola Popstars, alimsindikiza rafiki yake (Zubeda) ambaye hakutokea. Wakati anasubiri wahusika walimwambia aimbe tu lakini akaonyesha maajabu na akachaguliwa. Top 6 wallinia yeye, Langa, Witness, Illu, Terrence na Enika.
- Alipata Scholarship na kwenda kusoma Sanaa (Art & Design) Washington DC, Marekani. Ni mchoraji wa picha. “Nachora kila kitu”.
- Jina lake Shaa alipewa na marehemu Ngwair. Jina Shaa lilitoka kwenye jina (WAKILISHA) aliongeza A mwishoni na kuwa Shaa.
- Alikuwa msanii wa kwanza wa kike kusainiwa kwenye lebo ya Mj Records.
- Mwanzoni Master J alikuwa akimchana na kuhisi hakustahili kushinda mashindano ya Popstars. Anasema hiyo ilimjenga na kumtengeneza kuwa msanii mzuri.
Unaweza kusikiliza mahojiano yote ya Shaa katika kipindi cha Chill n Sky hapa:
Chanzo: Bongo5.com




Leave your comment