TANZANIA: Ben Pol aja na remix ya ‘Ningefanyaje’

 

Msanii wa muziki wa R&B Ben Pol hivi karibuni alitoa kibao chake kiitwacho ‘Ningefanyaje’ aliyoshirikiana na Avril pamoja na Rossie. Kibao hicho ambacho kinazidi kufanya viizuri katika anga za kimataifa katika chati za Top 10 za East na Rox za kituo cha SoundCity Tv cha nchini Nigeria pamoja na MTV Base. Ben Pol kaamua kuitolea remix yake ambapo ndani yake kashirikisha msanii kutoka Nigeria ambaye ni rappa aitwae Vj Adams amabae pia ni mtangazaji wa kituo cha SoundCity pamoja na msanii kutoka kundi la Weusi Gnako. Nyimbo hiyo imetayarisha na kuandaliwa na prodyuza aitwaye Erasto Machine.

 

Unaweza kuisikiliza nyimbo hii hapa:

Leave your comment