TANZANIA: Diamond kumtoa msanii mwingine
15 March 2016

Msanii mwenye kipawa cha aina yake na mwenye uwezo wa kuteka mashabiki ndani na nje ya mipaka ya Afrika Naseeb Abdul ali maarufu kama Diamond Platnumz anampango wa kumtoa msanii mwingine katika lebo yake ya Wasafi Classic Baby ‘WCB’. Hapo mwanzo msanii huyo alimtoa Harmonize katika tasnia ya kimuziki na kufanya vizuri na nyinbo zake kama ‘Aiyola’ na ‘Bado’ ambazo zinafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya muziki.

Diamond akiwa na Harmonize
Taarifa hizo za Diamond kumtoa msanii mwinine zimetokea mara baada ya msanii huyo kupost kupitia kurasa za Twitter na kuandika: “Panapo majaaliwa jumatano hii WCB Wasafi tutamtambulisha rasmi kijana mwingine mpya.. tafadhali wadau tunaomba sana support zenu” aliandika Diamond.

Alipost taarifa hiyo hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuzidi kufafanua na kusema: “Wengi wetu tumezaliwa katika familia duni na ndiomaana kidogo tunachokipata ni vyema kukitumia kusaidia wenzetu ili nao kesho wawainue na wengine... tafadhali wadau tunaomba sana mtusaidie kuwasupport vijana wenzetu.....Maana Sisi wenyewe kwa wenyewe ndio wakunyanyuana




Leave your comment