TANZANIA: Ben Pol kutoa nyimbo na msanii wa Nigeria

 

Msanii wa muziki wa R&B Ben pol amesema kuwa jumanne hii anatarajia kuachia kolabo yake mpya akiwa na rapa wa Nigeria. Akizungumza na Bongo5 jumatatu hii Ben Pol amesema kazi hiyo ataanza kutoa audio huku akiangalia uwezekano wa kutoa video. “Kazi tayari imekamilika na kesho inatoka, sitaki kuizungumzia kiundani Zaidi ila mashabii wangu wajue kesho watapata ladha mpya ya muziki wangu”, alisema Ben Pol.

Ben Pol kwa sasa anafanya vizuri na nyimbo yake iitwayo “Ningefanyaje” ambao unachezwa katika kubwa za kimataifa.

Kama hukupata nafasi ya kuitazama video ya 'Ningefanyaje' ya Ben Pol aliyoshirikiana na Avril pamoja na Rossie hii hapa:

 

Leave your comment