TANZANIA: “Niko tayari kuanza kufanya movie” - Shaa
14 March 2016

Msanii wa muziki wa bongo fleva nchini, Sarah Kaisi ‘Shaa’ amesema kuwa yuko tayari kuanza kufanya movie. Akizungumza na Bongo5, Shaa amesema kuwa alikuwa akishwishiwa kuingia kwenye filamu na muongozaji wa ‘Homecoming’, Seko Shamte akingie kwenye filamu. “Seko amenikalisha vikao viwili vitatu akiniconvince kuwa actress. Kwahiyo akanishawishi again for a movie or anything, I won’t say NO”, amesema Shaa.
“Niliwahi kufwatwa hapo nyuma nifanye movie akini nikakataa, miaka kama mitan[o sita iliyopita. Nahisi nilikataa kwasababu ya stori nilizokuwa nazisikia hakuna malipo mazuri kwahiyo nikawa naona kama mara mia ifanye muziki kwani unalipa vizuri fasta kuliko movies.”
Shaa ametoka kufanya media tour kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania kupromote nyimbo zake hususani nyimbo ya Toba uliotoka mwishoni mwa mwaka jana.

Kama ulipitwa na video ya Shaa 'Toba' unaweza kuitazama hapa:
Chanzo: Bongo5.com




Leave your comment