TANZANIA: Diamond ndiye baba halali wa Tiffa.

 

 

Msanii anayeitambulisha vizuri Tanzania katika anga za kimataifa, Naseeb Abdul hivi karibuni amewanyamazisha midomo wale waliomdhania kuwwa yeye sio baba halali wa Latiffa.

Msanii huyo pamoja na mkewe Zari Hassan, walilazimika kusafiri hadi Afrika Kusini kufanya vipimo hivyo kwani ni tetesi nyingi zilisikika kuwa Diamond si baba mzazi wa mtoto huyo.

Vipimo vilionyesha kuwa Diamond Platnumz ndiye baba halali wa Latiffa Dangote. Diamond aliangukwa na machozi mengi baada ya kupata majibu hayo, Kilichokuwa kinamuuma zaidi ni kwamba tetesi zilisikika na kusema kuwa inawezekana motto huyo akawa ni wa mume wa zamani wa Zari, Ivan Ssemwaga.

Damond alipoulizwa ni kwanini alilia pale alipopokea majibu hayo, alijibu akisema kuwa,”Kulia haikuwa tatizo. Ulitegemea ningefanyaje wakati wakupokea majibu niliyokuwa nikiyasubiri kwa dhati? Hasa kwa kipindi hiki ambacho jamii wanadhani mimi sio baba halali wa Latiffa?”.

Leave your comment