TANZANIA: Dogo janja aliniletea nyimbo 20 kabla ya 'My Life' - Madee
13 March 2016

Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection Madee Ali, alisema Dogo Janja alimletea nyimbo zaidi ya 20 kabla ya kuuchagua ‘My Life’, ambao amedai kuwa huo ndio unaondana na soko.
Akizungumza na Bongo 5 ijumaa hii Madee amesema amefanya yote kumpata Dogo Janja mpya.
“Unajua muziki aliokuwa akifanya Dogo Janja mwanzo , ulikuwa wa mkumbo Flani hivi, kwahiyo watu wakaimba imba sana muziki huo.”
“Sasa alivyokaa kwa muda mrefu nilikuwa natafakari, the way atavyorudi. Nikawa nawaza na kusema kuwa arudi kwa mtindo wa zamani wasingemwelewa. Dogo Janja ameniletea nyimbo zaidi ya 20, kila siku anarekodi lakini namwambia bado. Aliponiletea ‘My Life’ nikasema hapa safi, tukaedit kidogo, ngoma ikatoka,” alisema Madee.
Pia made amesema anajipanga kuachia video ya wimbo huo hivi karibuni.
Chanzo: Bongo5.com




Leave your comment