TANZANIA: Najma akanusha kutoka na Baraka Da prince
11 March 2016

Msanii Wa bongo fleva NAJ amefunguka na kuvunja ukimya na kusema kuwa yeye hana mahusiano yoyote ya kimapenzi na msanii Baraka da Prince. Baada ya kuenea habari kuwa anatoka kimpenzi na msanii huyo na kusisitiza kuwa Baraka ni rafiki yake wa karibu na hakuna zaidi.
Ukiangalia vizuri picha hizo hapa chin utagundua msichana anayeonekana kushoto akiwa na Baraka da prince amesuka mtindo kama anavyo onekana Naj kulia hapo.

Sasa wataalamu wa mambo wakaligundua hili na kusema huenda Naj na Baraka wana mahusiano ya kimapenzi kutokana na mfanano huo.
Akizungumza na Planet Bongo ya East Afrika Radio Naj amesema huyo siyo yeye ila ni msichana anayefanana naye kwa kuwa wapo wasichana wengi wanaosuka mtindo kama huo. Najma (21) amekanusha kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Baraka Da Prince na kuongeza kuwa ni wao ni washkaji tu.

Baraka Da Prince na Najma
Kwa upande wake Baraka Da Prince amesema msichana ambaye amempost siyo Naj ila ni mschana ambaye ndiye mpenzi wake na aliamua kumpost ili kukata ngebe za waliokuwa wanajitangaza kuwa naye kimahusiano.barakaBaraka aliwahi kusema msichana aliyenaye siyo maarufu hata kidogo na hajawahi kuwa na mahusiano na mtu maarufu zaidi ya kuwa marafiki huku akikili kuwa yeye na Naj ni washikaji tu.




Leave your comment