TANZANIA: Roma aanika mapenzi yake kwa mzazi mwenzake

 

Roma mkatoliki akijibu kupitia kituo cha redio cha e.fm katika kipindi cha ubaoni kinacho endeshwa na Gadner G Habash alipo ulizwa kuhusu kuonekana kwa picha kuwa ameoa, Roma amekubali madai hayo. Ingawa alisema zile ni taratibu za awali katika ndoa kama zilivyo ndoa nyingine na zile picha zilikuwa za send off.

 

 

Roma amedumu na mke mtarajiwa kwa miaka mitano na kubahatika kupata mtoto mmoja anae fahamika kwa jina la “IVAN” ambae mtoto huyo ali mtungia nyimbo ya 2030 iliyotoka miaka mitatu iliyopita. Roma amesema ndoa hiyo itafanyika mkoani kwake Tanga hivi karibuni na pindi akifika watu watafahamu.

 

PICHA ZAKE NA ZABIBU KIBA? Kuna picha zilisambaa kupitia mitandao ya kijamii ziki muonesha roma akiwa na “Zabibu salehe Kiba” sehemu tatanishi roma amekataa tuhuma hizo na kusema picha ilipigwa katika stuo za ‘Tongwe record’ na siku hiyo zabibu alikuwepo hapo wala haimaanishi chochote kati yao.

 

NYIMBO YA VIVA ALIMUIMBIA NANI? Roma alitoa ngoma ambayo ilikuwa tatanishi kipindi cha uchaguzi na baadhi ya redio ikiwemo e.fm walimueleza kuwa wasingeweza kuipiga roma ameitetea nyimbo hiyo iitwayo “VIVA” kuwa haikuwa inafungamana na chama chochote kwani mashairi yake yalikuwa kama maswali mfano ametolea mfano alipo sema “mwaka huu kombe linaenda monduli au kwa magufuli?”

Roma ameongeza kuwa aliwahi kutishwa kutokana na ngoma zake zinazo ichana serikali sana lakini hakuogopa kwakuwa alichokuwa ana kisema kina lengo la kuijenga jamii

Roma kitaaluma ni mwalimu aliwahi kufundisha baadhi ya shule, masoma aliyo fundisha ni hesabu na sayansi ambapo kwa maelezo yake aliacha baada ya kuona hakuna masilahi hivyo kujikita katika muziki.

 

Chanzo: Mtembezi.com

Leave your comment