TANZANIA: Manager wa Diamond asema Rich Mavoko hajasign WCB

 

Kumekuwepo na taarifa kwamba msanii wa bongofleva Rich Mavoco amechukuliwa na sasa kazi zake zitakua zinasimamiwa na lebo ya Diamond Platnumz ‘WCB’ na aliyenukuliwa akisema hivyo ni Harmonize ambaye ni msanii wa WCB.

 

 

Jorge Mendez 'Sallam SK' akiwa na Diamond Platnumz

 

Hata hivyo Diamond Platnumz kwenye Exclusive Interview na OnAIR with Millard Ayo wiki kadhaa zilizopita alisema miongoni mwa mipango mikubwa aliyokuwa nayo ilikua ni kumsaini Rich Mavoko kwenye lebo ya WCB ila bado mipango ilikua haijakamilika.

Sasa baada ya stori za leo kutoka kwamba imethibitishwa Mavoko kasainiwa WBC, meneja wa Diamond Platnumz Sallam alichukua time yake kumjibu mmoja wa watu waliomuandikia kwenye Twitter na kusema ‘Mavoko hajasainiwa WCB bado, ila Harmonize ameona kuwa Rich alikuwa na mazungumzo na viongozi akajua ni tayari. ukweli ni kwamba haja sign’

Rich Mavoko

Leave your comment