TANZANIA: Vanessa Mdee na Cindy Sanyu wawapagawisha mashabiki wao

 

 

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa raggae dancehall, Cindy Sanyu na Vanessa Mdee a.k.a V-Money waliwachanganya mashabiki wao Katika tamasha la kuhamasisha wanawake lililofanyika usiku wa tarehe 7 March katika ukumbi wa Club Play nchini Uganda.

Ilipofika mida ya saa tano usiku mashabiki walifurika kwa idadi kubwa wakishaherekea siku ya wanawake duniani. Mida ya saa saba ndiyo ilikuwa mwisho wa tamasha hilo ambalo limefana kwa onyesho la nguvu ambapo Cindy alitangulia kutumbuiza kwa nyimbo zake kama ‘Dillema’, ‘Sample Dat’ na ‘Ayokyayokya’ na baadae Navio alipanda jukwaani na kujiunga nae na kutumbuiza nyimbo walioshirikiana iitwayo ‘Ndimukkodo’.

 

 

Baada ya Cindy alifwata Vanessa Mdee akiwa na wanenguaji wake ambapo alifanya shoo kali na kuwatumbuisha mashabiki zake kwa nyimbo zake kali.

 

 

Tamasha hilo lilihudhuriwa na mastaa wengine kama , Michael Ross, Iryn Namubiru, Judith Heard, The Mith, Rajiv Rupareria, Hellen Lukoma, Angella Katatumba na aliyekuwa Miss Uganda 2015/2016 Zahara Muhammad

 

Rajiv Ruperaria

 

Angela Katatumba (Kushoto) akiwa na Iryn Namubiru

 

Mc Deedan

 

Michael Ross akiwa na Vanessa Mdee

 

Leave your comment