TANZANIA: “Namuona Nikclass mbali baada ya mwaka mmoja” - Hascana

 

Muongozaji wa nyimbo na mshindi wa tuzo za watu 2015, Hascana amesema Director Nikclass aliyetengeneza video mpya shika adabu yako ya Nay wa Mitego ndiye aliyekuja kwa kasi kutokana na kazi zake.

Hascana

 

Akizungumza na Bongo5 Jumamosi hii amesema Nikclass ni moja kati ya directors wakali wenye uwezo mkubwa wa kuchanganya picha. “Kusema kweli kuna huyu jamaa anaitwa Nikclass, mimi namuona mbali sana baada yam waka mmoja”, alisema Hascana. “Ukiangalia video zake nyingi utaona ni nini anafanyaga kwenye kazi zake, picha kali, anachanganya vizuri matukio. Yaanikwa ufupi mimi vijana ambao nawatabiria mambo makubwa ni huyu jamaa” aliongeza.

Hata hivyo Bongo5 ilimtafuta director huyo ambaye pia alitengeneza video ya Kamikaze ‘Shori’ na kuzungumzia kauli hiyo ya Hascana. “Kusema kweli kama amesema hivyo nashukuru Mungu, kawsababu ni moja kati ya director mkubwa kwa sasa. Binafsi nimefurahi sana na pia ni chanagamoto katika kazi zangu, kuongeza bidi pamoja na kuwa mbunifu. Kwahiyo mimi naahidi sitamuangusha yeye pamoja na mashabiki w kazi zangu”, alisema Nikclass.

Nikclass hivi karibuni amechukua tuzo ya Best Director katika tuzo za Nyambago Central Tanzania, zilizofanyika huko Dodoma.

 

Tazama hapa moja kati ya kazi za Nicklass: Nay Wa Mitego "Shika Adabu Yako".

 

Chanzo: Bongo5.com

Leave your comment