TANZANIA: Rich Mavoko ndani ya WCB!!

 

 

Harmonize

 

Hitmaker wa ‘Bado’ Harmonize amevunja ukimya baada ya kufunguka kuhusu ujio wa msanii mwenye sauti ya kuvutia ambaye anafanya vizuri na wimbo wake wa Naimani Rich Mavoko kwenye lebo ya WCB, huku akifanya vyema pia kwenye kiitikio (Chorus) cha wimbo wa msanii wa Hip Hop Darasa uitwao ‘Kama Utanipenda’, ambao umetokea kupendwa na watu wengi, na kupelekea video yake kuanza kuchezwa kwenye kituo cha Trace Tv.

 

Rich Mavoko

 

Rich Mavoko hivi karibuni zilizuka tetesi kuwa Hitmaker huyo wa ‘Naimani’ atakuwa amehamia kwenye Lebo ya muziki ya Wasafi Classic Baby (WCB) iliyo chini ya msanii mahiri anae ipeperusha vyema bendera ya Tanzania Diamond Plutnumz.

Msanii Harmonize ambaye pia yupo kwenye Lebo hiyo ya WCB ameweka wazi kuhusu ujio wa Rich Mavoko kwenye Lebo yao na kueleza kuwa, uwepo wake WCB utamsaidia kupanua wigo wake wa kisanaa kwenye soko la nje, na kongeza kuwa msanii mwenye kipaji kama Rich Mavoko anahitaji menejimenti ya kueleweka kama ilivyo WCB, huku akiahidi kuwepo kwa ladha tofauti kutokana na wakali hao kufanya kazi ndani ya Lebo moja.

Chanzo: Mtembezi.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Leave your comment