TANZANIA: “Masaki Theory” – Brian Simba

Tasnia ya muziki nchini Tanzania imezidi kukua kwa kasi ya ajabu. Wasanii kama Diamond Platnums, Joh Makini, Fid Q na wengine wamekua wakiitambulisha vyema muziki wa bongo fleva pamoja na hip hop kiujumla katika anga mbalimbali za kimataifa.Hivyo basi imepelekea hata wasanii chipukizi kuwa na Imani na muziki wakiwa na mategemeo ya kufika mbali.

Brian Simba

 

Mfahamu Brian Simba, Mwanamuziki mpya, wa kizazi kipya cha nchini Tanzania ambaye amejikita katika muziki wa rap. Amekuwa akitengeneza nyimbo kwa muda mrefu. Hivi sasa anawajia na orodha nyimbo kumi iitwayo ‘Masaki Theory”. Brian Simba katika nyimbo zake kwenye albamu yake hii ya ‘Masaki Theory’ amefanya kazi na maprodyuza kama Brakxxx, RDG, Domi Beats, Kiqo na Salaam Status. Katika nyimbo zake hizo ameshirikisha wasanii kama Topher Jaxx, George Gavin, Brakxx, Chuche, Avid na Fresh like Uuh.

Hizi ndiyo nyimbo zinazopatikana katika albamu ya 'Masaki Theory':

Wapo mastaa wa nchini waliokubali na kupenda kazi zake kama Vanessa Mdee na OsseGreca Sinare na kupost katika account zao za twitter.

 

 

Unaweza kusikiliza nyimbo hizo hapa:

Leave your comment