TANZANIA: "Nina imani katika ubora wa kazi kuliko umaarufu" - Fid Q
4 March 2016
Kolabo ni kitu muhimu kwa msanii, kwa sababu humfanya kupanua wigo wa kazi zakekutambulika zaidi kutokana na msanii anaefanya nae kolabo, tumeona wasanii wengi wa Bongo wakifanya kolabo na wasanii mashughuli katika nchi mbalimbali ikiwemo Afrika Kusini, Nigeria, Kenya, Uganda na nje ya hapo wakiwa na matumaini yale yale ya kutoboa pande hizo.
Kwa upande wake msanii nguli wa Hip Hop hapa nchini Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q ana mtazamo tofauti dhidi ya kolabo mbalimbali za wasanii na watu mashughuli, huku akiamini uwezo wa mtu kufanya kazi kuliko umaarufu wake.
Akizungumza hivi karibuni katika kipindi kipindi cha XXL kinachorushwa na Clouds FM staa huyo amesema kuwa ana amini katika ubora wa kazi kuliko umaarufu wa msanii anae fanya nae kolabo ndio maana kolabo zake nyingi za nje amefanya na watu ambao sio maarufu ikiwemo ngoma yake mpya ya Walk It Off aliyo mshirikisha msanii Taz kutoka Zambia.
Chanzo: mtembezi.com





Leave your comment