TANZANIA: ‘Sina tatizo na Nay’- Shetta

 

Msanii wa muziki wa hip hop Shetta au kwa jina lengine anafahamika kama Baba Kayla amefunguka katika kipindi cha East Africa Radio jumatano hii, alifunguka na kusema kuwa hana tatizo na Nay wa Mitego. “Hiyo kwangu ni kama kichekesho , kwasababu huyo Nay mwenyewe anajua jua alichokifanya ni kama kichekesho kwangu  siyo issue kwangu kuichukulia kama tatizo sababu ukweli wote yeye anajua. Sisi ni kama familia ndiyo maana umeona nimepost video yake. This is my car ndiyo maana yeye kasema labda umuulize Shetta sababu yeye hajui”, alisema Shetta.

Mbali na kuimba Shetta alisema kuwa yeye pia ni mfanyabiashara. Anapata maendeleo na pesa za kutosha ndiyo maana anauwezo wa kumiliki gari kama hilo.

Nay Wa Mitego

 

"Mimi nafanya mitikasi yangu, mimi ni mfanyabiashara na mwanamuziki hivyo napiga show za kutosha na bado nahustle sana, hivyo nina kila sababu ya kupata maendeleo na maendeleo ndiyo haya sasa, hivyo sioni kama ni tatizo lna wala sioni kama amenisema nilikuwa najua toka before lakini pia mimi ndiyo mwenye mamlaka ya kila mtu na hakuna mwingine”.

 

 

Leave your comment