TANZANIA: Ruby afunguka kuhusu Ali Kiba

Hivi karibuni msanii wa nyimbo za bongo Fleva Hellen Majeshi ‘Ruby’ alishambuliwa na baadhi ya mashabiki wa msanii Ali Kiba , baada ya msanii huyo kumfananisha na mbwa katika mahojiano yake katika kipindi cha The Spora Show.

Katika studio za Bongo 5 msanii huyo alipoulizwa kuhusiana na swala hilo alijibu na kusema,” Ni kwamba Bro ‘Ali Kiba’ hakunikosea chochote, hakuniita mimi mbwa kama inavyosemekana kwa watu kama  ‘mbwa mbwa’, watu ndio wanajaribu kutengeneza beef, lakini mimi yule jamaa sina chuki na hakuniita hivyo” amesema Ruby.

“Watu wake wa karibu ndiyo wanaofahamu kwahiyo the way walivyodefine nje huko, ilifanya kuleta maana nyingine,  kwamba bro ulimaanisha hivi nilivyoelewa au ni vile! Kwahiyo mimi nilifanya kama kuuliza lakini sio kumlaumu  kwanini, ni jinsi watu  walivyopokea” alisema Ruby.

Aliendelea na kusema ,“Walitakiwa kusoma kile nilichokiandika , ila kwasababu wamekurupuka siwezi kuwalaumu.” Ruby alisema hana mazoea na Ali Kiba kwakuwa hawakutani lakini hana tatizo nae na kwamba kama ikatokea wakafanya kazi, watafanya tu.

Leave your comment