TANZANIA: Baraka Da Prince ajibu baada ya kudaiwa kutelekeza mtoto
2 March 2016

Baraka Da Prince
Msanii wa muziki ya Bongo Fleva Baraka Da Prince, anayetamba na nyimbo kama ‘Siachni nawe’ pamoja ‘Nivumilie” aliyomshirikisha Rubby, hivi karibuni alituhumiwa kwa kutelekeza mtoto.
Msichana ambaye ndiye mama wa mtoto alikiambia kipindi cha ‘YOU HEARD’ cha Clouds kinachotangazwa na Soudy Brown, alikiambia kituo hicho na kusema kuwa, ” Tatizo sasa hatoi huduma ya mtoto, yani kila siku nikimpigia simu yuko busy anadai yuko studio na huku nyumbani kwetu wananifukuza wanadai niende Dar es salaam.”
Baada ya tuhuma hizo alitafutwa Baraka Da Prince n kujibu kwa kusema kuwa,” ‘Kwanza siwezi kumkataa wala kumtelekeza mtoto, ni kweli mimi nina mtoto na taarifa za kuwa sitoi matumizi ya mwanangu. Sijawahi kupewa taarifa za matumizi ya mwanangu na nikaachi kutuma, imeniumiza sana, na hii imeniuma kuliko kitu chochote kilichowahi kuniuma katika maisha yangu”,alisema Baraka.




Leave your comment