TANZANIA: B.O.B inarudi tena -Nyandu Tozi

Msanii wa hiphop Nyandu Tozi amesema kuwa kundi la B.O.B linarudi tena kwa kukaa kimya kwa muda mrefu na kuhakikisha kuwa kundi hilo halitakaa kimya tena bali litaendelea na mashambulizi ya kimuziki katika tasnia hii ya Sanaa.

Katika mahojiano yake na Radio Ras ya Dodoma, Nyandu Tozi alisema kuwa,” Kwanza tunamshukuru Mungu mwaka tumeuona vizuri na crew tunaisongesha vizuri. Hadi sasa tumeshafanya ngoma mbili na tuna ratiba ya kufanya ngoma nne au sita kwa mwaka huu, tupo serious Zaidi, sio kama mashabiki wetu walivyotuzoea kwa mwaka ngoma mara moja. Walikua wakilalamika ila kwa safari hii hatutakaa kimya tutaachia video nne, na ngoma mbili tutaachia bila video. Mashabiki wetu wasubirie kazi zetu.

Leave your comment