TANZANIA:Producer Hascana kurudisha nyimbo za zamani.

Kutokana na ulimwengu kukua kila kukicha, na teknolojia kushika kasi kati maisha yetu ya kila siku, Producer anaekuja kwa kasi Hascana ameamua kurudisha nyimbo ambazo zilishawahi kuhit kipindi cha zamani na kutaka kuzileta katika ulimwengu wa sasa. Kwa kuanzia Hascana ameamua kuanza na nyimbo ya Dully akiwa na Temba 'Ndiyo yeye'.

"Nimeamua kushoot nyimbo zilizowahi kuhit miaka ya nyuma na kuzifanya ziwe katika muonekano wa sasa", ameandika Hascana katika mtandao wa Instagram.

"Kila baada ya miezi 3 nitakua naachia video ya nyimbo moja amayo ilishawahi kuhit miaka hiyo, nimeanzan na ya Mh.Temba ft Dully Sykes. Je ni nyimbo gani unayopendekeza kifwate baada ya hii?" alisema Hascana.

Leave your comment