TANZANIA: 'Achia body' yazidi kumpandisha Ommy Dimpoz
1 March 2016

Mwishoni mwa mwaka jana nyota wa muziki wa kizazi kipya, Ommy Dimpoz alizindua video ya wimbo wa ‘Achia Body’ ambao anasema kuwa sasa inazidi kukata mawimbi kwa kurushwa katika televisheni za nje, ikiwamo Trace Tv ya Nigeria na Ufaransa.
Ommy Dimpoz amezidi kueleza kuwa Trace Urban walishatangaza kurusha video ya wimbo huo mfululizo kwa wiki nzima kitu ambacho kinaonyeshwa kwenye runinga hiyo na imeikubali kazi yake hiyo.
”Wimbo huo kama zilivyo nyingine nilizowahi kutoa,ulianza kukubalika taratibu na sasa unazidi kufanya vizuri hadi kupenya katika Televisheni za nje ya nchi, hii ni fahari kwangu na kwa mashabiki wangu.”Ommy Dimpoz.

Vilevile hitmaker huyo wa 'Achia Body' ameeleza kuwa wapo baadhi ya mashabiki wenye mtindo wa kuhukumu nyimbo mpya kwa muda mfupi kabla ya kuzipa muda na kuzielewa vyema.




Leave your comment