TANZANIA: Baba wa Diamond ajipanga kumuona Mjukuu wake Tiffah kwa mara ya kwanza

Hatimaye baba wa msanii gwiji  anayetamba Afrika wa miondoko ya Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameruhusiwa kumuona mjukuu wake Tiffah.

Ni baada ya mvutano wa huku na huku kutokana na tofauti zao, kwa sasa wawili hao wamemaliza tofauti zao na kumfanya mzee  Abdul Juma kuwa na sababu ya kufurahi tena.

Kwa mujibu wa Global Publisher, wamesema Diamond amemsamehe baba yake na kumruhusu kuweza kumuona mama mtoto wake (Zari) na mjukuu wake Tiffah.

“Baba Diamond hana kinyongo  wameshazungumza na mama Diamond wameshamaliza tofauti zao, Diamond mwenyewe hana tatizo kilichobaki ni kwenda tu kule kufanya dua”, kilisema chanzo cha Global Publisher.

Diamond na mzee wake hawakuwa na maelewano baada ya kuwatelekeza mama yake na ndugu zake katika umri mdogo kutokana na mambo ya kifamilia.

 

 

Leave your comment